Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) leo amekabdihi ripoti ya ukaguzi wa Vyama vya Ushirika yam waka 2018/2019 kwa Kamishina Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbung’o katika Ofisi za Wizara ya Kilimo, Mtumba Jijini Dodoma.
Mhe. Hasunga amesema ukaguzi uliofanywa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) umebaini ubadhilifu wa zaidi ya shilingi Bilioni 124.5 ambapo umefanywa na Vyama Vikuu vya Ushirikia, Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS), Vyama vya Msingi vya Mazao (AMCOS) ambapo jumla ya vilivyokaguliwa ni hadi tarehe 30 Juni 2019 ni 11,410 kati ya Vyama hivyo, Vyama hai ni 6,463; Vyama Sinzia ni 2,844 na Vyama ambavyo havipatikani 2,103.
Kutokana na maagizo hayo, hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2019 COASCO ilikagua Vyama vya Ushirika vipatavyo 4,413 sawa na asilimia 102.63 ya lengo la Serikali la kukagua Vyama 4,300.
Katika vyama hivyo 4,413 vilivyokaguliwa, vyama 303 (6.87%) vilipata Hati inayoridhisha, Vyama 2,378 (53.89%) vilipata Hati yenye shaka, Vyama 879 (19.92%) vilipata Hati isiyoridhisha na Vyama 853 (19.32%) vilipata Hati mbaya.
Waziri Hasunga alisema kuwa Kati ya Vyama Vikuu 38, Vyama 4 vilipata Hati Safi, Vyama 22 vilipata Hati yenye shaka, 9 vilipata hati isiyoridhisha na 3 hati mbaya. Vyama hivyo Vikuu 3 vilivyopata HATI MBAYA inayohusisha hoja zenye viashiria vya ubadhirifu wenye Jumla ya shillingi 856,357,955 kwa RUNALI, SCCULT 4,878,662,431 na KYECU kwa kukosekana kwa hati za kuhesabu mali za kudumu mwisho wa mwaka.
Alisema kuwa Chama Kilele (Shirikisho-TFC) kimepata Hati Isiyoridhisha ambayo inajumuisha fedha benki zisizofanyiwa malinganisho na pia kutooneshwa katika taarifa za fedha kiasi cha shilling 1,538,726,787
Kati ya Vyama vya Ushirika wa Mazao (AMCOS) 2,710 vilivyokaguliwa, vyama 15 vilipata Hati Safi, 1347 Hati yenye Shaka, 599 Hati Isiyoridhisha na vyama 749 vilipata Hati Mbaya. Matatizo makuu katika vyama hivyo vya AMCOS ni kushindwa kuandika vitabu vya hesabu, malipo mengi kutokuwa na vielelezo vya malipo, mifumo dhaifu ya udhibiti wa makusanyo na mauzo ya mazao kukosekana