Naibu Waziri akutana na Mkuu wa FAO

Mheshimiwa Mavunde na Mkuu wa FAO Qu Dongyu

Naibu Waziri wa Kilimo wa Tanzania , Mhe. Anthony Mavunde, wakati kikao cha 32 cha Shirika la Chakula na Kilimo(FAO) upande wa Afrika kinachoendelea Jijini Malabo,Equatorial Guinea amepata nafasi ya kufanya kikao na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani(FAO) Ndg. Qu Dongyu

Mhe. Mavunde aliwasilisha vipaumbele vya Wizara ya Kilimo katika kuifikia Agenda 10/30 na kutaka kuendelea kuimarisha ushirikiano na FAO katika kufikia malengo hayo. Maongezi hayo yalijikita katika mambo yafuatayo.

1. Kukuza uwezo wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) ili kutimiza malengo yake ya utafiti na uvumbuzi wa mbegu bora na kanuni bora za kilimo ili kuwawezesha wakulima wetu kulima kwa tija.

2. Uzalishaji mkubwa wa mbegu bora kupitia Wakala wa Mbegu Tanzania (ASA) na sekta binafsi kwa lengo la kupunguza utegemezi wa kuagiza mbegu nje ya nchi na badala yake kuifanya Tanzania mzalishaji mkubwa wa mbegu zinazitosheleza mahitaji ya nchi na kuuzwa nje ya nchi.

3.Uwekezaji kwenye Kilimo cha Umwagiliaji ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa lengo la kupunguza utegemezi wa kilimo cha mvua amabcho kimekuwa kikiathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi.

4.Kuimarisha huduma za ugani kwa kuwezesha mafunzo maalum ya zao moja moja ili kuongeza umahiri wa maafisa ugani katika kuwahudumia wakulima na kuwasaidia kulima kwa tija.

5.Mpango wa ushirikishwaji wa Vijana katika kilimo kupitia mfumo wa mashamba makubwa ya pamoja(Block farms).

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa