Mwelekeo wa kilimo chetu kwa sasa ni umwagiliaji – Waziri Bashe

Tanzania Agriculture Minister Hussein Bashe

Kipaumbele cha Serikali ya Tanzania ni kuimarisha Sekta ya Kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza utegemea wa mvua. Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe aliyazungumza hayo mkoani Morogoro wakati alipofungua mkutano wa Wadau wa kilimo cha umwagiliaji ulioandaliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tarehe Juni 15, 2022.

Waziri Bashe alisema kwenye bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka 2022/2023, serikali imetenga shilingi bilioni 364 katika kujenga na kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji maji mashamba madogo na makubwa; Huku kukiwa na ongezeko la bilioni 50 ambazo zimetengwa ili kuendeleza umwagiliaji.

Waziri aliongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ako na utashi wa kisiasa katika Sekta ya Kilimo; Serikali imedhamiria kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji.

“Serikali imetenga hekta elfu 20 kwa ajili ya mashamba ya Vijana ambayo yatajengwa miundombinu ya umwagiliaji ili kupunguza tatizo la ajira. Tumefungua milango kwa Wadau wa Sekta ya Kilimo kutupa mawazo yatakayoleta matokeo chanya,” alisema Waziri Bashe.

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa