Wanafunzi wa kilimo wasifukuzwe – Kusaya

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ameagiza uongozi wa Chuo cha mafunzo ya Kilimo na Mifugo ( MAMRE) cha Wanging’ombe mkoani Njombe kutowafukuza wanafunzi wanaoshindwa kulipa ada ya mafunzo.Kusaya ametoa agizo hilo alipofanya ziara kukagua maendeleo ya chuo hicho na kuongea na wanafunzi na kusema uongozi wa chuo utafute njia rafiki kuwasaidia wanafunzi wenye mazingira magumu yanayosababisha kutolipa ada kwa muda .

” Vyuo vyote 29 ( 14 vya serikali na 15 vya binafsi) ni vyangu kwani vinalenga kuzalisha maafisa ugani watakaokwenda kuhudumia wakulima nchini.Nitaendelela kuvisaidia bila kuangalia nani anakimiliki muhimu vitoe mafunzo bora kwa wanafunzi wa kitanzania” alisema Kusaya

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo ameahidi kutoa kompyuta ili kuwezesha kuanzisha maktaba mtandao ( e- learning) na kugharimia mwanafunzi mmoja kwenda kujifunza kanuni bora za ufugaji kuku kisasa katika chuo cha Ihemi Iringa kwa gharama za serikali.

Katibu Mkuu amesema katika kuboresha mafunzo kwa vitendo atakipatia Chuo hicho Kitalu nyumba moja ( Green House) ili wafundishe klimo cha mbogamboga na matunda (horticulture )

Chuo cha MAMRE kina wanafunzi 103 wa ngazi ya astashahada na stashahada.Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Geofrey Mapesa alisema changamoto kubwa Kwa sasa ni kukosekana kwa mfumo wa udahili wa pamoja ( Central Admission System) hali inayopelekea upungufu wa wanafunzi.

Tayari wanafunzi 169 wamehitimu mafunzo ya kilimo na mifugo tangu chuo hicho kilipoanzishwa mwaka 2014 chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe.

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa