Vijana washauriwa kuwekeza kwa kilimo

Mhe. Omari Mgumba Naibu Waziri Kilimo wa Tanzania amewataka vijana kuwekeza katika uzalishaji mbegu ili kuondoa upungufu wa mbegu bora nchini.” Mahitaji ya mbegu nchini ni tani 187,197 wakati uzalishaji ni tani 71,000 hivyo kuna fursa kubwa katika uzalishaji mbegu kwa vijana nchini.

Mhe.Omari Mgumba pia amezishauri Halmashauri zote nchini kuyabaini na Kuyahakiki mashamba pori na kuyatolea mapendekezo namna ya kuyagawa kwa vijana ili waweze kuendeleza kazi za kilimo, Ushauri huo ameutoa akiwa Mkoani Njombe kwenye kongamano la vijana.

Pia amewataka wakulima wote nchini kujisajili kwenye daftari la Wakulima ili kupata takwimu sahihi zitakazo saidia kupeleka huduma kwa wakulima.

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa