Ukaguzi kuhusu mpunga Tanzania

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amewaongoza Makatibu Wakuu wa Wizara za Viwanda na Biashara Prof Riziki Shemdoe,Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw.Gerald Mweli na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Balozi Joseph Sokoine leo 22 Aprili 2020 kufanya ukaguzi wa pamoja wa utekelezaji wa mradi wa kuongeza uzalishaji wa zao Mpunga (ERPP) mkoani Morogoro.Awali wakikagua mradi wa ujenzi wa ghala la kuhifadhia mpunga kijiji cha Mvumi wilaya ya Kilosa viongozi hao wameonesha kuridhishwa na hatua iliyofikiwa kwenye mradi huo.”Tumeridhishwa na hatua ya asilimia 99 ya ujenzi wa ghala kukamilika hivyo fanyeni taratibu wakulima wakabidhiwe mapema mradi huu.” alisema Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Kusaya Mradi huo wa ghala Hadi sasa umegharimu shilingi milioni 735 kati ya milioni 971 ambapo utakuwa na uwezo wa kuhifadhi mpunga tani 1300 kwa mwaka na kukoboa mpunga kilo 1200 kwa siku.

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa