Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe. Hussein Bashe akiwa katika maonyesho ya kimataifa ya Dubai Expo 2020, yanayoendelea ameongoza mkutano mkubwa unaotangaza mazao ya kilimo ya Tanzanja na fursa za uwekezaji katika sekta ya Kilimo(Tanzania Agri Business and Investment Forum).
Amewaambia jumuiya ya kimataifa kuwa Tanzania imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya kilimo, na kwamba iko ardhi hekta milioni 40 inayofaa kwa kilimo na hekta milioni 29 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, hivyo wigo wa uwekezaji kwenye kilimo ni mkubwa.
“Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan ameelekeza benki zote nchini kutoa mikopo ya kilimo chini ya asilimia kumi ili kumsaidia mkulima na kila anayefanya kazi katika mnyororo wa thamani kwenye mazao ya kilimo” AlisemaMkutano huo uliowakutanisha wafanyabiashara wa sekta ya Kilimo Tanzania na wa kutoka nchi mbalimbali duniani.
Pia, amehudhuria mkutano wa Mawaziri wa Kilimo kutoka Afrika wakijadili hali ya sekta ya kilimo na usalama wa chakula. Aidha,amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji mbalimbali wenye nia na lengo la kuwekeza katika sekta ya kilimo nchini Tanzania. Tanzania ni moja kati ya nchi 192 zinazoshiriki katika maonyesho hayo.