Taasisi za kifedha Tanzania kuhimizwa kuongeza uwekezanji katika kilimo

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ameeleza umuhimu wa taasisi za kifedha kuongeza uwekezaji katika Kilimo na kupunguza masharti ili mkulima aweze kukopa zaidi
Amesema Kilimo hakitakuwa kwa haraka kama inavyotegemewa na serikali haitaweza kufikia malengo endapo uwekezaji katika sekta ya Kilimo utabaki chini.
Maelezo hayo aliyatoa wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa ms ekwa ulioko ndani ya ya majengo ya bunge la jamhuri ya muungano ambapo wadau hao walitoa mawasilisho mbalimbali juu ya kuongeza uwekezaji katika kilimo.


Aidha mkutano uliwakutanisha wadau wa Sekta ya Kilimo ambao ni  Benki ya Kilimo (TADB) ,Benki ya CRDB Benki ya,NMB, Kamati ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji,Kamati ya bunge ya bajeti, Shirika la Kilimo Afirika (AGRA),Mtandao wa wakulima wadogo Tanzania (MVIWATA), SAGCOT, na Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo.
Akiongea wakati wa mkutano huo Mhe. Bashe amesema kwamba asilimia mia moja (100%) ya mikopo inayotolewa na benki ni asilimia nane tu (8%) zinaelekezwa katika sekta ya Kilimo kiasi ambacho ni kidogo sana kwa kuinua sekta.


Kiwango hicho cha asilimia 8 huelekezwa katika Kilimo, asilimia 92 inaenda kwenye sekta ambazo hazihusiki na Kilimo wakati asilimia 75 ya watanzania wanategemea kilimo. Zaidi ya asilimia 85 ya chakula katika Tanzania kinatokana na kilimo. Uwekezaji mkubwa unatakiwa ufanyike ili Kilimo kiendelee kuzalisha malighafi ya viwanda, alisema Mhe. Bashe
“Uwekezaji huo unatakiwa kuanzia shambani mpaka sokoni ili mkulima aweze kuuza mazao yake. Katika kukabiliana na hali hii tumeona ni vyema kukutana na ninyi wadau wetu katika sekta ya Kilimo kuona namna ya kumsaidia mkulima kuweza kupata mkopo kwa ajili ya kilimo,” alisema Bashe

1R6A6531


Aidha Mhe. Bashe amewataka wadau wa sekta ya fedha waliohudhuria kikao hicho kujadili namna ambavyo wataweza kusaidia Kilimo kiweze kukua , kwani Kilimo hakiwezi kukua kama hakuna uwekezaji wa kutosha.
Lengo kubwa la kuitisha mkkutano huo ni kuona namna ambavyo sekta ya fedha itasaidia sekta ya Kilimo katika kutoa mikopo kwa bei nafuu na kwa kiwango kikubwa ikilinganisha na wanavyotoa kwa sasa.
Akiwasilisha andiko lake katika mkkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Maendeleo ya Kilimo amesema kwamba “Kabla hatujaanza kufikiria namna ya kuboresha mkopo kwa mkulima, tufikirie kwanza je huyu mkulima ameandaliwa vipi katika kupata mkopo huo na ameshapata elimu ya kutosha kuhusiana na mkopo?,”


Hii inaonesha kwamba wakulima wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na pia kinachofanya mkopo kupungua katika sekta hiyo. Hata hivyo ameendelea kusema kwamba katika zao la tumbaku hawakupata shida kwani kiwango cha mkopo kilichochukuliwa kilirejeshwa kwa muda uliostahili.
Naye mwenyeki wa kamati ya bunge ya Kilimo maji na mifugo Mahamudi Mgimwa amesema uwekezaji katika Kilimo ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda.
“Hatuwezi kufanikiwa kwenye sekta ya Kilimo kama hatujawekeza vizuri kwenye Kilimo ambacho kinahitaji mitaji mikubwa,” alisema Mhe. Mgimwa.
Hata hivyo Mhe. Mgimwa amesisitiza taasisi za benki kupunguza makato kwa wakulima na kuwashauri kuongeza mitandao ya kibenki ili iweze kuwafikia wakulima wote nchini.
Mwanyekiti huyo ameikumbusha sekta binafsi kutumia fursa ya kuwekeza kwenye Kilimo hasa katika wakati huu ambao serikali imepunguza bajeti kwenye sekta ya kilimo.
Akiongea wakati wa wasilisho lake Prof David Nyange ambaye ni mshauri wa mambo ya Sera toka wizara ya Kilimo amesema kwamba sekta ya Kilimo imeendelea kukua kwa asilimia tatu (3%) hivyo kufanya ukuaji wa maskini kukuwa kwa wastani.
Amesema kuna umuhimu wa kuwekeza kwenye sekta ya Kilimo na kwenye sekta ya viwanda hasa viwanda vya uchakataji wa mazao ya Kilimo ili kuweza kushusha kasi ya ukuaji wa umaskini.
Pof ameongeza kwamba kasi ya ukuaji wa usalama wa chakula imekuwa kubwa hivyo kupunga kazi ya ukuaji wa kasi ya utapiamlo,
Utapiamlo umekuwa ukishuka kwa slimia 1% kwa mwaka wakati umaskini umekuwa ukishuka kwa asilimia 0.5% kwa mwaka hivyo itachukua miaka 30 kuondoa utapiamlo hapa nchini na miaka 50 kuondoa umaskini hapa nchini kama uwekezaji hautafanyika kwenye sekta ya kilimo, alisema Prof. Nyangi.

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa