Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe. Hussein Bashe ametoa miezi sita kwa wazalishaji wa Miche ya mazao mbalimbali ambao hawajasajiliwa kwenye mfumo wa usimamizi wa ubora wa Miche na vipando kufutiwa uzalishaji.
Alisema jijini Dodoma alipokuwa akizindua kongamano la uzinduzi wa mfumo wa usimamizi wa ubora wa miche na vipando. Waziri Bashe aliwataka wadau wa Sekta ya Kilimo kuchangamkia fursa kwakuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha utashi wa kisiasa katika kuinua Sekta hiyo.
Aidha, Waziri Bashe alisema serikali kwa sasa itaipa kipaumbele Sekta ya Mazao ya Matunda na Mbogamboga. Vilevile ameongeza na kusema kuwa Serikali itaanza kuandaa utaratibu wa bora kuotesha mbegu za Asili ili ziweze kuwa na tija kubwa kwenye Kilimo.