Naibu Waziri Bashe akutana na wadau wa shahiri na zabibu Dodoma

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amekutana na wadau wa zao la shahiri na zabibu kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo katika sekta ndogo ya Zabibu na kukubaliana namna ya kutekeleza . Mkutano huo ulihudhuriwa na wanunuzi wa zao la zabibu na shahiri  pamoja  na wakulima wa mazao hayo.

Mhe. Bashe amesema kuwa kwa sasa wakulima wa shahiri hawana soko, hivyo ni vyema kukubaliana kwa msimu ujao wakulima walime shahiri. Hata hivyo Bashe amekitaka kiwanda cha Tanzania Breweries (TBL)  kukifungua  au kukikodisha kiwanda cha Kilimanjaro ambacho kipo mikononi mwao ili kianze kazi.

Aidha, Mhe. Bashe ameeleza kwa msimu huu wa sasa wakulima hawajalima zao la shahiri hivyo hakuna malighafi  ya zao hilo. Ili wakulima waweze kulima kwa msimu ujao  Wizara itahakikisha mikataba inakuwa sawa kwa pande zote mbili  kwa mnunuzi na kwa mkulima na kuwataka wakuu wa wilaya, wakuu wa mkoa na warajis wa vyama vya ushirika watakapo saini mikataba hiyo na Serikali iione.

Mkurugenzi wa Tanzania Bruweries (TBL)  Bw.Philip Redman amesema kwa msimu  ujao  wa 2021,wameingia mkataba na wakulima 300 na kiwanda kina uwezo wa kuchukua tani 5,000 kwa mwaka.  Hata hivyo  TBL inatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata shahiri  tani 32 jijini Dodoma alisema Bashe.

Kwa upande wa  Serengeti Breweries (SBL) Mkurugenzi wa Mahusiano  Bw.John Wanyancha amesema kuwa kwa msimu ujao wanatarajia kuchukua tani 3,000 kwa wakulima 60. Aidha, Bashe amewataka wakulima kutotegemea zao moja bali wajikite pia kwenye mazao mengine na kuitaka kampuni kununua shahiri kwa wakulima wote hao.

Kwa zao la Zabibu Mhe.Bashe amesema  msimu wa kilimo unaanza mwezi wa nane hivyo Serikali inahitaji uhakika wa masoko na wanunuzi wanatakiwa kusema namna ambavyo watanunua zabibu hizo.

“Hatutaki wakulima wa zabibu mwezi wa nane wakati wa kuvuna wapate shida ya masoko na nahitaji kujua kwa mwezi huo tutavuna kiasi gani . Njia pekee itakayotusaidia ni kuingia mkataba na wakulima” alisema Bashe

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi.Theresia Mahongo amesema zao hili ni zao la kibiashara linalowaingizia uchumi wakulima   na ametoa ombi kwa wanunuzi kuongeza tani kwa zao la shahiri kwani wakulima wanalima zaidi ya tani  8,000 zinazohitajika.

Naye Mkulima wa shahiri Bw. Domisiani William kutoka Karatu amesema changamoto wanazokumbana nazo  ni mapato na bei ndogo ya zao. Pia ameiomba Serikali kuongeza tani kwani wakulima wanalima zaidi.

Katika mkutano huo makubaliano yaliyofikiwa ni kwamba kwa msimu ujao wakulima wa shahiri warudi shambani, mikataba iwe ya uwazi ili Serikali iweze kuiona, Kiwanda cha shahiri cha Kilimanjaro kifunguliwe, wakulima wa shahiri wanatakiwa kuheshimu viwango na ubora na uwekezaji mkubwa  wa kiwanda utawekwa Dodoma wa Dola Miliioni 200 wenye uwezo wa kuchakata tani 32,000, Zabibu inayozalishwa ndani iweze kununuliwa, kukuza mfumo wa mkataba wa zabibu, kuwe na specification kati ya anayezalisha na anayechukua mchuzi wa wine,Wale waliokiuka mradi wa chamwino watachukuliwa hatua na kuwa na mkataba wa makubaliano kwa wanunuzi wakubwa na wadogo.

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa