Mwaka huu Tanzania tumejipanga kusindika korosho nyingi zaidi – Waziri Hasunga

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga amewaambia Wasindikaji wadogo na Wakubwa wa korosho kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuongeza kiwango kikubwa cha usindikaji kuliko ilivyokuwa mwaka jana na kwamba Serikali haitanunua tena korosho bali itaweka mazingira mazuri kwa Wafanyabiashara kununua zao hilo kutoka kwa Wakulima bila ya kuwalalia.

Mhe Hasunga ameyasema hayo katika mkutano wake maaalum alioutisha leo tarehe 9 Septemba 2019 katika ofisi za Wizara ya Kilimo Dodoma lengo likiwa ni kuzungumza na Wasindikaji hao ili kujiandaa na msimu mpya wa ununuzi wa korosho ambapo taarifa rasmi ya Wizara itatolewa na wiki ijayo.

Waziri Hasunga amesema licha ya Serikali kuendelea na azma yake ya kuongeza thamani ya zao la korosho kwa kuwasisitiza Wabanguaji kuongeza ukubwa wa mazao ya korosho kwa kusindika zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita.

Tumeona kabla ya kutangaza taarifa rasmi ya Wizara yenye kuzindua rasmi msimu mpya wa ununuzi wa korosho, ni vyema tukutane nanyi Wadau ili kujadiliana namna nzuri ya kuboresha biashara ya korosho kwa lengo la manufaa ya Wakulima wetu” Amekaririwa Waziri Hasunga

Katika hotuba yake; Waziri Hasunga ameelekeza kuwa Wabanguaji hao kutoa Taarifa kwa Wizara kwa msimu wa kilimo wa 2019/2020 katika maeneo kadhaa ikiwemo teknolojia wanazotumia katika ubanguaji na usindikaji wa korosho, uwezo wa mashine zao kusindika kwa mwaka, idadi ya Wafanyakazi walioajiliwa katika viwanda, uwezo wa viwanda kubangua na kusindika korosho kwa mwezi na mwaka na mapendekezo ya bei ya kununulia kabla ya msimu kuanza.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa Wasindikaji pia wanapaswa kuwa wa wazi katika kuishauri Serikali namna nzuri ya kuboresha zoezi zima la ununuzi mpya wa korosho na kueleza changamoto wanazokutana nazo.

Awali katika taarifa yake, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Bwana Francis Alfred amesema uzalishaji wa korosho kwa msimu huu unataraji kufikia tani laki 3 na nusu (350,000) na kuongeza kuwa tija itaongezeka ikiwa sehemu kubwa ya uzalishaji itabanguliwa na kusindikwa hapa hapa nchini.

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa