Mikoa inayolima zao la Pamba wakutana Tanzania

Wakuu wa mikoa inayolima zao la pamba nchini wamekutana kupokea na kujadili taarifa ya kamati ndogo kuhusu changamoto zinazoikabili na kutoa mapendekezo ya utatuzi wake.

Kamati ndogo ya wadau iliundwa Octoba mwaka jana jijini Mwanza kwa lengo la kuja na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto za zao hilo nchini.

Akifungua kikao hicho katika ukumbi wa Hazina Dodoma, Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kikao hicho ni muhimu ili kutengeneza mustakabari mzuri wa tasnia ya pamba kwenye mikoa 17 inayolima zao hilo. Bashe amesema msimu ujao wa kilimo cha pamba unapaswa uwe mzuri na usiwe na matatizo licha ya mikoa michache bado kuwa na takribani asilimia 20 ya pamba isiyonunuliwa hadi sasa.

“Pamba na kilimo ni biashara tusipeleke siasa.Msimu huu ulikuwa mgumu.Tumekubalia serikalini kuwa biashara hii ifanywe kwa uwazi zaidi ili mkulima apate manufaa ya jasho lake” alisema Bashe. Naibu Waziri Bashe amesema Wizara ya Kilimo mkakati wa miaka mitano kuhusu sekta ndogo ya pamba ili kukidhi mahitaji ya soko na upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima nchini.Bashe aliongeza kusema tayari wizara imefanya majadiliano na wizara za Viwanda na Biashara na ile ya Fedha na Mipango juu ya mustakabali wa zao hili msimu ujao

“Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2020 imeelekeza ushirika kusimamia sekta ya pamba kwa manufaa ya wakulima nchini,hivyo lazima tutafute suluhu ya changamoto za masoko “ alisisitiza Bashe. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya wadau wa pamba Adamu Malima alisema ni wakati sasa wizara ya Kilimo ikaweka mikakati mahsusi ya uparikanaji wa bei nzuri ya pamba ya wakulima kupitia mfumo wa ushirika.“Ushirika nchini lazima uwe na takwimu sahihi za wakulima,kiasi cha pembejeo kinachotakiwa na eneo linalolimwa ili kuepusha hasara kwa wakulima kubebeshwa madeni yasiyo wahusu” alisema Malima.

Mkuu wa Mkoa Malima amebainisha kuwa suala la utata na ugani kwenye zao la pamba ni muhimu lipewe kipaumbele lakini wizara ya kilimo haioneshi jitihada.Mkuu wa mkoa Malima alisema Wizara ya Kilimo inatakiwa pia kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo za pamba kwa wakati na zenye ubora kuhakikisha zinawafikia kwa wakati na bei nafuu.

Kikao hiki maalum cha wadau kilihudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya Mara,Simiyu,Morogoro,Kagera,Kigoma,Singida,Mwanza,Geita,Shinyanga,Kilimanjaro,na Katavi.

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa