Naibu Waziri wa Kilimo Tanzania Mhe. Anthony Mavunde amewataka wakulima nchini kujitokeza katika zoezi la usajili wa wakulima ili serikali iweze kuhudumiwa kiurahisi kwa nyanja tofauti tofauti kwenye shughuli zao za Kilimo.
Naibu Waziri Mavunde aliyasema hayo tarehe 27 Oktoba 2022 kwenye mkutano wa hadhara uliohusisha mawaziri nane wa kisekta wanaoshughulikia migogoro ya ardhi kwa vijiji 975, uliofanyika kijiji cha Mpanga wilaya ya Wang’ing’ombe mkoani Njombe.
“Najua hapa nyinyi asilimia kubwa ni wakulima, na maeneo ambayo mtagawiwa hapa mtayatumia kama mashamba ili kuendeleza sekta ya kilimo.
Mhe Rais anatamani kujua idadi ya wakulima alionao Tanzania, ili aweze kuwahudumia kwa urahisi. Kwahiyo niwaombe mjitokeze katika zoezi linaloendelea mjisajili, ili Serikali ijue namna ya kufikisha huduma mbalimbali na kusaidia kutatua changamoto za msingi zinazomkabilli mkulima wa Tanzania. Hivyo wakulima wa Wanging’ombe nichukue fursa hii kuwaomba mtumie nafasi hii kujisajili ili sasa hizi fursa zinazotamkwa kwenye kilimo na wewe iwe rahisi kunufaika. Ni dhamira ya Mhe. Rais, kuona wakulima wanapata huduma mbali mbali hasa za ugani ili mwisho wa siku mkulima huyu alime kwa tija na kilimo chake kilete mafanikio katika maisha ya mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla,” alisema Mavunde.
Kamati hii ya kisekta ya mawaziri nane inaendelea na ziara zake za utatuzi wa mgogoro wa ardhi