AfriFARM waja na Technolojia ya kupambana na kiwavijeshi Vamizi Tanzania

Share on facebook
Share on twitter
Share on whatsapp
Share on email

Shirika la Kimarekani linalojihusisha na miradi mbalimbali ya kilimo na elimu (project concern international) PCI leo wamewasilisha matokeo ya matumizi ya mfumo wa Afrifarm katika kupambana na kiwavijeshi vamizi fall armyworms katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kilimo IV Uliopo Dodoma na kuhusisha wataalamu mbalimbali na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Kilimo .

Mfumo huo ambao hutumika Zaidi kwenye simu ganja uliogunduliwa na Shirila la PCI kwa lengo la kupambana na kiwavijeshi vyamizi katika Mkoa wa Mara ikihusisha kutoa mafunzo ya utambuzi wa kiwavijeshi vamizi (FAW identification) ,ukaguzi wa mashamba, FAW field scouting na kutoa taarifa za kiwango cha mashambulizi katika ngazi ya jamii husika

Akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao hicho mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya kilimo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango sehemu ya Ukusanyaji wa Taqwimu Bwana… ..Rubboa amesema shirika hilo kwa kushirikiana na Kitengo cha Huduma ya Afya ya Mimea (PHS) chini ya Wizara ya Kilimo, Kampuni ya Dimag walifikia hatua kubwa ya kuvumbua mfumo huo wakielekitroniki unaoitwa AfriFARM, (Africa fall armyworm Response Mechanism).

FB IMG 1568997057142

Akiuelezea mfumo huo Bwana Luboa amesema kwamba AfriFARM ni mfumo wa simu (mobile phone application) uliobuniwa ili kumuwezesha Afisa ugani au mkulima kujifunza juu ya ufahamu wa kiwavijeshi vamizi, ukaguzi wa shamba na mbinu mbalimbali za kukabiliana na uvamizi huo.

Aidha shirika la PCI limewekeza katika kukuza matumizi ya teknolojia ambapo lilifanya majaribio katika Kata 45 zilizoko katika wilaya ya Butiama, Bunda na Musoma vijijni katika Mkoa wa Mara ambako kulipata athari ya visumbufu vamizi alisema Bwana luboa.

Hata hivyo Bwana Rubuo ametoa wito kwa wataalamu walioshiriki katika mkutano huo kuahakikisha wanatoa michango yao katika kuimarisha mfumo huo ambao utasaidia kuimarisha usalama wa chakula hapa nchini.

Naye Meneja wa Idara ya Kilimo Bwana Amithay Kuhanda Amesema wameshirikiana na Wizara ya Kilimo katika kupambana na kiwavijeshi vyamizi ambao wanachangia kushusha kiwango cha uzalishaji wa mazao ya wakulima.

Anasema kuwa wanapambana na kiwavijeshi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki simu janja ambao una saidia kufanya ufutiliaji wa mashamba yaliovamiwa na kiwavijeshi na kutoa taarifa kupitia mfumo wa simu hiyo.

Mfumo huu unafanya kazi zaidi kuanzia ngazi za Kata kufikisha taarifa ngazi ya wilaya kwa haraka zaidi hiyo kusaidia kutoa taarifa sahihi za maeneo ambayo yameathirika kwa hatua zaidi.

Mchango washirika hili la PIC ni kuandaa mfumo ambao unasaidia kuwa tambua viwavijeshi na kufikisha taarifa haraka kwa wataalamu na watoa maamuzi kwa maaana ya serikali alisema bwana Amithay Kuhanda.

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa