Tanzania -Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kutoa shilingi milioni 500 kwa serikali

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo imetoa mchango wake wa shilingi milioni 500 kwa Serikali mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ambaye aliambatana na Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na Msajiri wa Hazina Bwana Athumani Mbuttuka.

FB IMG 1578504831969

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema mchango wa shilingi milioni 500 zilizotolewa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo kwenye hafla ya makabidhiano ya michango na magawio kutoka kwa Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali kimeonyesha kuwa Taasisi hiyo inajiendesha kwa faida na tija; na kwamba inapaswa kupongezwa.
Dkt. Mpango ameyasema hayo wakati wa hotuba yake, baada ya kupokea gawio na michango ya fedha zilizotolewa kwa Serikali kutoka kwa Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi 13 za Serikali kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kilimanjaro katika Jengo la Wizara ya Fedha, Jijini Dodoma.

Akiongea wakati wa hafla hiyo ya makibidhiano ya hundi za mfano, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema inatia moyo kuona Wenyeviti wa Bodi pamoja na Wakuu wa Taasisi, Wakala na Mifuko na Vyuo vya Elimu ya Juu ambao wameo gawiwo na michango yao kwa Serikali, yenye jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 2.
“Kwa niaba ya Serikali, ninawashukuru kwa kuitikia wito wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, nataka niwahakikishe kuwa fedha hizi, zitarudi kwa ajili ya kuendelea kuwatumikia Watanzania wanyonge”. Amekarirwa Waziri Mpango.
“Wito wangu na matarajio yangu ni kuwa mwaka ujao, mtajiangalia zaidi ili tupate zaidi kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi wetu”.
Waziri Mpango ameongeza kuwa kwa sasa duniani nchi zilizokuwa zikitoa misaada kupitia Mfuko Mkuu wa Dunia (Global Fund) hazifanyi hivyo, zaidi zimejikita katika kutoa misaada hiyo kwa nchi zao zaidi na kwamba ndiyo maana ni lazima nchi zinazoendelea kama Tanzania zijifunge mkanda kwa kutumia rasilimali zao.
“Misaada siku hizi imepungua, ni aibu kwa Baba mwenye nyumba, kwenda kwa Wakubwa na kuanza kuombaomba, n

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa