Vikundi vya kijamii 38 kutoka wadi za Hindi, Mkunumbi,Bahari na Witu katika kaunti ya Lamu nchini Kenya zimepokea hundi ya zaidi ya shilingi milioni 23 Kutoka Kwa mradi wa Kenya Climate Smart Agriculture kupitia Idara ya Kilimo Kaunti ya Lamu.

Akikabidhi rasmi hundi hizo,Gavana Fahim Twaha, amewashauri waliofaidi na pesa hizo kuzitumia vizuri ili kusaidia kaunti ya Lamu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Aidha Twaha, amesema vikundi vilivyofanikiwa kupata pesa hizo wawe ni kielelezo Kwa vikundi vengine.

Naye Naibu Gavana Abdulhakim Aboud ambaye ni Waziri wa Kilimo,amesema mikakati imewekwa ili kudhibiti pesa hizo.
Vikundi hivyo vitaekeza katika kilimo cha korocho, pamba,kuku,maziwa na samaki.
Mradi huu unaofadhiliwa na Banki ya Ulimwengu ulianza mwaka 2017 hadi 2022.