Vyuo vya mafunzo ya kilimo kufunguliwa Tanzania

A bulb onion. Photo by Kimuri Mwangi

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald M. Kusaya anawatangazia Wanafunzi WOTE waVyuo vya Mafunzo ya Kilimo (MATI) chini ya Wizara ya Kilimo kuwa vyuo vimefunguliwa rasmi siku ya Jumatatu, tarehe 01 Juni, 2020.Wanafunzi wote wanatakiwa kuwepo vyuoni kuendelea na masomo baada ya agizo la Serikali kutaka vyuo vifunguliwe.

Aidha, Wakuu wa Vyuo vyote 14 vya Mafunzo ya Kilimo (MATIs) wanaagizwa kufanya maboresho ya kalenda ya masomo kwa kuzingatia maagizo ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) yaliyotolewa tarehe 22 Mei, 2020.Wanafunzi, Wakufunzi pamoja na watumishi wasio walimu mnakumbushwa kutilia maanani maagizo ya Serikali juu ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa COVID – 19.

Share your views about this story

Related stories

Subscribe to Kilimo News

Get the latest agriculture news in East Africa