Ili kuimarisha idadi na matumizi ya nyama nyeupe, serikali ya kaunti ya Uasin Gishu imegawia wakulima kupitia vyama vya ushirika samaki wachanga 20,000 wa kufugwa.
Hatua hii itahakikisha kwamba wanafuga samaki wengi na kuibua ushindani wa kibiashara kati yao.
Waziri wa kilimo Samuel Yego akishirikiana na afisa mkuu wa maendeleo ya mifugo Barnabas Too pamoja na mkurugenzi wa idara ya Samaki Charles Mwaniki wamewanasihi wakulima kukuza samaki kwa makini kwa kuwa wakiwa wachanga ni dhaifu.
Wamewataka kuhakikisha mabwawa ya samaki yamezingirwa vilivyo ili kuzuia uharibifu.Aidha Waziri Yego amewatahadharisha wakulima dhidi ya kulisha samaki wachanga vyakula kiholela na kuwataka kuzingatia malisho kwa wakati unaofaa kulingana na maagizo ya maafisa.